Home Habari Kuu Mlanguzi wa mihadarati akamatwa Mombasa

Mlanguzi wa mihadarati akamatwa Mombasa

Mshukiwa huyo Zuher Ali Mohamed, alikamatwa katika msako uliotekelezwa na maafisa wa polisi, baada ya kupashwa habari na wananchi.

0
Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati Zuher Ali Mohamed.

Maafisa wa polisi wa kukabiliana na ulanguzi wa mihadarati katika kaunti ya Mombasa, wamemkamata mlanguzi wa dawa za kulevya katika mtaa wa Kiembeni, eneo la Bombo,  Kisauni.

Mshukiwa huyo Zuher Ali Mohamed, alikamatwa katika msako uliotekelezwa na maafisa wa polisi, baada ya kupashwa habari na wananchi.

Wakati wa msako huo, pakiti kadhaa za dawa za kulevya aina ya heroin na bangi, zilipatikana katika nyumba na gari za mshukiwa.

Gari la mshukiwa huyo pia lilinaswa likiaminika kuwa lilinunuliwa na fedha za ulanguzi wa mihadarati, pesa taslimu shilingi 26,250 na dola 200 za Marekani, mashini ya kupima uzani, karatasi za kupakia na simu tatu za rununu.

Mshukiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakama ya Mombasa leo Alhamisi, kufunguliwa mashtaka.

Website | + posts