Home Kimataifa Mkutano wa 6 wa UN kuhusu mazingira waanza Nairobi

Mkutano wa 6 wa UN kuhusu mazingira waanza Nairobi

0
kra

Mkutano wa sita wa Umoja wa Mataifa, UN kuhusu mazingira umeanza leo Jumatatu, Februari 26, 2024 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira, UNEP, Gigiri, Nairobi.

Washiriki wapatao elfu 5 kutoka mataifa 193 wanachama wa UN  wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na viongozi kadhaa wa nchi mbalimbali.

kra

Mkutano huo wa siku tano utakaofikia tamati Machi 1, 2024 unatarajiwa kujadili mada mbalimbali chini ya mandhari, “Hatua za pande zote ambazo ni faafu, jumuishi na endelevu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kupotea kwa viumbe hai na uchafuzi”.

Kilele chake kitakuwa tamko la mawaziri kuhusu namna ya kusonga mbele.

Kongamano hilo ambalo ni kuu katika kuunda sera kuhusu mazingira, UNEA, linalenga kurejesha maelewano kati ya binadamu na mazingira na hivyo kuboresha maisha ya watu walio katika hatari kubwa.

Ni fursa pia kwa serikali za nchi mbalimbali, makundi ya uanaharakati, wanasayansi na sekta ya kibinafsi kupaza sauti na kuhusishwa katika kutunga sera ya ulimwengu mzima kuhusu mazingira.

Awamu ya awali ambayo ni ya 5 ya kongamano la UNEA iliandaliwa Nairobi ambapo mikutano ilikuwa miwili tofauti kutokana na masharti ya kuzuia kuenea kwa virusi vya korona.

Mkutano wa kwanza ulifanyika kwa njia ya mtandao kutoka Nairobi Februari 22 na 23,2021 huku wa pili ukiandaliwa Nairobi pia Februari 28 hadi Machi 2, 2022.

Website | + posts