Home Habari Kuu Mkurugenzi wa KBC Samuel Maina aongoza upanzi wa miti Meru

Mkurugenzi wa KBC Samuel Maina aongoza upanzi wa miti Meru

0

Wafanyakazi wa shirika la Utangazaji Nchini, KBC wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Samuel Maina, wameshiriki shughuli ya upanzi wa miti katika kituo cha Marania, kaunti ya Embu mapema leo Jumatatu.

Shughuli hiyo inalandana na wito wa kitaifa wa serikali kuwataka Wakenya wote kupanda miti siku ya Jumatatu, Novemba 13, ambayo imetangazwa kuwa sikukuu.

Mwanachama wa Bodi ya KBC Joe Mathai akipanda mti katika kituo cha Marania

Maina aliandamana na mwanachama wa bodi ya KBC Joe Mathai, wafanyakazi pamoja na wakazi wa Meru katika shughuli hiyo.

Ni shughuli inayokusudia kupiga jeki lengo la serikali kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032.

Wakati wa sikukuu ya upanzi wa miti leo Jumatatu, serikali inakusudia kupanda miti milioni 500.

Lengo ni kutumia kipindi cha mvua inayonyesha kote nchini kwa sasa kuhakikisha miti hiyo inakua na kusaidia katika kukabiliana na suala sugu la mabadiliko ya tabia nchi ambalo limeikumba dunia katika siku za hivi karibuni.

Website | + posts