Home Habari Kuu Mkewe Mbunge Samuel Moroto amefariki

Mkewe Mbunge Samuel Moroto amefariki

0

Mary Saisy Moroto mke wa mbunge wa eneo la Kapenguria Samuel Moroto ameaga dunia. Mama huyo anasemekana kuaga dunia Ijumaa.

Moroto alitumia akaunti yake ya Facebook kutoa taarifa hiyo akieleza kwamba mke wake alikuwa akiugua ugonjwa wa Saratani.

Alisema kama familia wameumia sana na kuondokewa na mama huyo ambaye walijitolea kwa hali na mali kuokoa maisha yake bila mafanikio.

Mwakilishi wa kike wa kaunti ya Pokot Magharibi Rael Aleutum Kasiwai amemwomboleza mama Mary akimtaja kuwa mama aliyejitolea kwa majukumu yake na mwaminifu.

Rael aliitakiwa familia ya Moroto faraja wakati huu wa majonzi.

Website | + posts