Home Habari Kuu Mkewe Amos Kimunya afariki

Mkewe Amos Kimunya afariki

0

Mke wa mbunge wa zamani wa eneo la Kipipiri Amos Kimunya kwa jina Lucy, ameaga dunia. Alikata roho akiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi.

Kimunya amemwomboleza marehemu mke wake akimtaja kuwa nguzo muhimu katika maisha yake binafsi na kazi yake kisiasa.

Aliongeza kusema kwamba alichangia pakubwa katika mipango ya kutunza mazingira na alikuwa anaunga mkono makundi ya vijana na wanawake.

Kiongozi huyo wa zamani wa wengi bungeni ndiye alitangaza kifo cha mke wake kupitia taarifa ambapo alielezea kwamba aliaga saa tisa alfajiri.

Aliahidi kutangaza mipango ya mazishi baadaye.

Amos Kimunya hajakuwa akionekana sana katika jicho la umma tangu aliposhindwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita na Wanjiku Muhia wa chama cha UDA.

Website | + posts