Home Kimataifa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan ajiuzulu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan ajiuzulu

Kufikia sasa zaidi ya wakazi milioni tano wa taifa hilo, wamekoseshwa makazi, milioni moja kati yao wakiwa wakimbizi kwenye nchi jirani.

0

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes amejiuzulu miezi minne baada ya kuombwa na serikali hiyo kuondoka.

Kwenye hotuba yake ya mwisho, Perthers alikosoa jeshi la Sudan pamoja na kundi la kijeshi lenye silaha la Rapid Support Forces, RSF.

“Mzozo uliopo utaacha historia ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,” Perthes aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba takriban watu 5,000 wameuawa na wengine zaidi ya 12,000 kujeruhiwa tangu mapigano kati ya majenerali wawili hasimu kuzuka nchini Sudan, Aprili 15.

Kufikia sasa zaidi ya wakazi milioni tano wa taifa hilo, wamekoseshwa makazi, milioni moja kati yao wakiwa wakimbizi kwenye nchi jirani.

Ripoti zimeongeza kwamba suala linalotia wasi wasi zaidi ni mapigano ya kikabila yanayoendelea kuongezeka kwenye eneo la Darful.

Eneo hilo lilishuhudia ghasia za kikabila pamoja na ukatili dhidi ya binadamu mwanzoni mwa miaka ya 2000, wakati UN ukihofia kujirudia kwa hali hiyo.

Website | + posts
VOA
+ posts