Home Habari Kuu Mitihani ya KCPE na KPSEA yaingia siku ya pili

Mitihani ya KCPE na KPSEA yaingia siku ya pili

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu aliongoza shughuli ya ufunguzi wa kasha lililokuwa na mitihani ya KCPE katika kaunti ndogo ya Kibra, Jijini Nairobi.

0
Waziri wa elimu Ezekiel Machogu katika kaunti ndogo ya Kibra.

Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) na tathmini ya gredi ya sita (KPSEA), imeingia siku ya pili leo Jumanne, huku maafisa wakuu serikalini wakiongoza shughuli ya ufunguzi wa karatasi za mitihani.

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu aliongoza shughuli ya ufunguzi wa kasha lililokuwa na mitihani ya KCPE katika kaunti ndogo ya Kibra, Jijini Nairobi.

Baadaye waziri huyo alielekea katika shule ya msingi ya Olympic katika mtaa wa Kibra kuongoza shughuli ya ufunguzi wa mitihani.

Kwa upande mwingine,waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya dijitali Eliud Owalo, aliongoza ufunguzi na usambazaji wa mitihani  katika afisi ya naibu kamishna wa kaunti  wa Nairobi, mtaani Westlands.

Naye katibu wa elimu ya msingi Belio Kipsang alikuwa mjini Ngong kuongoza ufunguzi wa mitihani.

Serikali imewatuma maafisa 60,000 wa usalama kuhakikisha usalama na maadili ya mitihani.

Website | + posts