Home Habari Kuu Mishahara ya maafisa wa polisi kuongezwa kwa asilimia 40

Mishahara ya maafisa wa polisi kuongezwa kwa asilimia 40

Kiongozi wa taifa pia aliagiza kufanyiwa marekebisho kwa sheria na sera zinazoongoza utendakazi wa huduma ya taifa ya polisi, huduma ya magereza na huduma ya vijana ya taifa, kuhakikisha uwajibikaji na uwazi.

0

Maafisa wa huduma ya taifa ya polisi, wale wa magereza na maafisa wa huduma ya taifa ya vijana NYS, watapokea nyongeza ya mishahara ya asilimia 40 katika muda wa miaka mitatu ijayo

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi baada ya kupokea mapendekezo ya marekebisho katika sekta ya usalama kutoka kwa jopokazi linaloongozwa na David Maraga, Rais William Ruto, alisema  marekebisho hayo ya mishahara yatawapa motisha maafisa wa usalama.

“Marekebisho ya masharti ya Utendakazi kwa maafisa wa usalama, yatapandisha motisha yao na kubadilisha sekta ya usalama. Yataimarisha uwezo wetu wa kuwalinda wakenya, Mali yao, uhuru wao na kuleta mazingira bora ya uwekezaji na ukuzaji wa biashara,” alisema Rais Ruto.

Kiongozi wa taifa pia aliagiza kufanyiwa marekebisho kwa sheria na sera zinazoongoza utendakazi wa huduma ya taifa ya polisi, huduma ya magereza na huduma ya vijana ya taifa, kuhakikisha uwajibikaji na uwazi.

Jopokazi hilo linaloongozwa na Maraga, lilibumiwa tarehe 21 mwezi Disemba mwaka 2022, kutoa mapendekezo ya kuimarishwa kwa mazingira ya utendakazi wa maafisa wa usalama, na kupendekeza mageuzi ya sera na  sheria za maafisa hao.

Website | + posts