Home Burudani Mipango ya mazishi ya Junior Pope yatangazwa

Mipango ya mazishi ya Junior Pope yatangazwa

0
kiico

Familia ya mwigizaji wa Nigeria Johnpaul Obumneme Odonwodo, maarufu kama Junior Pope imetangaza mipango ya mazishi yake kupitia kwa bango lililosambazwa mitandaoni.

Marehemu Pope ataagwa kwa muda siku 4 kuanzia Jumatatu Mei 13, 2024 nyumbani kwao katika jimbo la Enugu nchini Nigeria.

Shughuli nzima itaanza na misa ambayo itahudhuriwa na watu wa familia yake na watu wa karibu ifuatiwe na kesha kwa ajili ya mashabiki wake wote pamoja na familia siku tatu baadaye.

Mwili wake utatolewa Ijumaa Mei 17, 2024 kwa umma kuutazama na kutoa heshima zao za mwisho na kuzikwa mara moja. Jumapili Mei 19, 2024 misa ya kutoa shukrani kwa ajili ya maisha yake itaandaliwa ili kukamilisha mpango mzima wa kumuaga.

Junior Pope na watu wengine watatu walikufa maji huko Asaba wakiwa katika harakati za kuandaa filamu pale ambapo dau lao lilizama.

Alifariki akiwa na umri wa miaka 43 na awali familia yake iilizua gumzo baada ya kutoa bango la kutangaza mipango ya mazishi ambalo halikugusia mkewe na watoto.

kiico