Home Burudani Millie Odhiambo amtetea Akothee

Millie Odhiambo amtetea Akothee

0

Mbunge wa eneo la Suba Kaskazini Millie Odhiambo amemtetea mwanamuziki Akothee baada yake kufichua kwamba hayuko tena kwenye ndoa miezi michache tu tangu afanye harusi.

Mabona alitumia mitandao ya kijamii ambapo alisema kwamba ataendelea kumshabikia Akothee iwe yuko na mumewe au hayuko naye au ameolewa zaidi ya mara hamsini.

Anamsifia kwa kile ambacho anasema kwamba ni kuweza kujiinua maishani na anaendelea kukua bila kuzingatia vikwazo vya aina yoyote.

Kiongozi huyo alishangaa kwamba Wakenya wanaangazia sana maisha ya mwanamuziki huyo ambaye haangazii maisha yao akisema ameweza kuwadhibiti kwa hilo.

Alimhimiza Akothee aolewe tena iwapo atapata mume mwingine awe tapeli au la akimhimiza amwalike kwa harusi.

Akothee amezungumziwa sana kwenye mitandao baada ya kuashiria kwamba ameachana na mume wake wa asili ya Uswizi ambaye alikuwa amempa jina la “Omosh”.

Aliondoa jina la jamaa huyo kwenye akaunti zake na kisha kuchapisha taarifa ndefu akielezea alivyokumbwa na msongo wa mawazo baada ya kugundua mambo mabaya kuhusu Omosh.

Mwimbaji huyo hakugusia aliyoyagundua ila aliahidi kuyafichua siku za usoni na akaomba wachapishaji taarifa mitandaoni wampatie muda.

Akothee alifanya harusi na Denis Schweizer almaarufu Omosh Aprili 10, 2023, hafla ambayo ilihudhuriwa na viongozi na watu maarufu akiwemo mkewe Waziri Mkuu wa zamani Ida Odinga.

Website | + posts