Home Habari Kuu Miili ya maafisa 2 wa KRA waliosombwa na mafuriko yaopolewa

Miili ya maafisa 2 wa KRA waliosombwa na mafuriko yaopolewa

0

Miili ya maafisa wawili wa Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru Nchini, KRA waliosombwa na mafuriko Ijumaa wiki  iliyopita imeopolewa.

Kulingana na vitengo vya uokozi vikiongozwa na kamishnaa wa kaunti ya Kwale Michael Meru, miili ya wawili hao ilipatikana jana Jumapili pamoja na mwili wa kijana mmoja wa bodaboda ambaye pia alisombwa Ijumaa.

Maafisa hao walikuwa safarini wakati gari walimokuwa wakisafiria liliposombwa wakijaribu kuvuka barabara iliyofurika karibu na mto.

Serikali za kaunti za Pwani zimetangaza mafuriko kuwa janga na kuwatahadharisha wakazi kuhamia maeneo yaliyo salama.

Mafuriko yanashuhudiwa katika kaunti 33 nchini zinazopokea mvua kubwa tangu mapema mwezi huu.