Home Habari Kuu Mikakati yawekwa kukabiliana na dawa ghushi nchini

Mikakati yawekwa kukabiliana na dawa ghushi nchini

Mkataba huo unalenga kuimarisha udhibiti na utekelezaji wa hakimiliki za bidhaa za afya.

0

Bodi ya kudhibiti dawa na sumu nchini imetia saini mkataba wa ushirikiano na halmashauri ya kupambana na bidhaa ghushi nchini kwa lengo la kukabiliana na dawa ghushi.

Mkataba huo unalenga kuimarisha udhibiti na utekelezaji wa hakimiliki za bidhaa za afya na teknolojia kwa lengo la kuzuia usambazaji wa bidhaa ghushi za afya nchini.

Afisa mkuu mtendaji wa bodi hiyo Dkt. Fred Siyoi na mwenzake wa halmashauri ya kukabiliana na bidhaa ghushi Dkt. Robi Mbugua, walielezea matumaini kuhusu mkataba huo wa kuimarisha utekelezaji wa hakimiliki katika sekta ya dawa.

Mkataba wa Maelewano unaonyesha mfumo wa kina unaojumuisha vipengele mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubadilishana habari, uchunguzi wa pamoja, utafiti, upatanishi wa udhibiti na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya mashirika.

Asasi hizo mbili zilisema mkakati huo ni muhimu katika kushughulikia changamoto zinazoletwa na kuimarika kwa teknolojia huku ikilinda ubora wa bidhaa za dawa na teknolojia humu nchini.

Website | + posts