Home Kimataifa Miili ya raia wa Israel yapatikana Gaza

Miili ya raia wa Israel yapatikana Gaza

Hamas ilikuwa imetishia kumuua mateka mmoja kwa kila wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiua raia bila ya onyo.

0

Miili ya baadhi ya raia wa Israel walionaswa na Hamas wakati wa shambulizi wiki moja iliyopita, imepatikana na jeshi la Israel wakati wa shambulio la ardhini Gaza siku ya Ijumaa, magazeti ya Israel yanaripoti.

Haaretz na Kituo cha Yerusalemu vilisema kuwa Jeshi la Ulinzi la Israeli lilipata idadi isiyojulikana ya miili, na kuirudisha katika eneo la Israeli.

Vikosi vya askari wa miguu na wenye silaha vilishiriki katika uvamizi huo ambapo seli ya Hamas ambayo ilirusha makombora ya vifaru katika eneo la Israeli “ilitolewa”, gazeti la Jerusalem Post linasema.

Takriban mateka 150 waliokamatwa na watu wenye silaha wa Hamas kutoka kusini mwa Israel Jumamosi iliyopita, wanaaminika kushikiliwa katika maeneo ya siri ndani ya Gaza. Miongoni mwao ni wanawake, watoto na wazee.

Hamas ilikuwa imetishia kumuua mateka mmoja kwa kila wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiua raia bila ya onyo.

Vyombo vya habari vya Israel vinaripoti kuwa wanajeshi waliokuwa wakivamia Gaza, walipata miili na mali za baadhi ya watu waliotoweka.