Home Kimataifa Miili mitano yapatikana gorofani katika kitongoji cha Paris cha Meaux

Miili mitano yapatikana gorofani katika kitongoji cha Paris cha Meaux

0

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wameanzisha uchunguzi wa mauaji baada ya miili mitano kupatikana katika mji wa kaskazini mashariki mwa Paris.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya ndani, waathiriwa ni mwanamke na watoto wake wanne wadogo.

Miili yao ilipatikana katika mji wa Meaux ulioko zaidi ya kilomita 41 kutoka mji mkuu wa Ufaransa.

Waligunduliwa katika ghorofa, mwendesha mashtaka wa eneo hilo aliliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Kulingana na tovuti ya habari ya Actu17, ambayo iliripoti kisa hicho kwa mara ya kwanza, polisi wanamsaka baba mwenye umri wa miaka 33, ambaye “amekimbia”.

Mwendesha mashtaka Jean-Baptiste Bladier alithibitisha kwa vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa idara ya polisi ya Versailles ilikuwa ikichunguza.

BBC
+ posts