Home Biashara Mifuko 522,000 ya mbolea ya bei nafuu yatolewa kwa wakulima

Mifuko 522,000 ya mbolea ya bei nafuu yatolewa kwa wakulima

0
kra

Serikali imewapatia wakulima mifuko 522,000 ya mbolea ya bei nafuu ili kupiga jeki shughuli za kilimo na hivyo kuhakikisha nchi hii ina chakula cha kutosha kukidhi mahitaji ya raia wake. 

Mbolea hiyo imetolewa kwa wakulima katika maeneo ya kati, mashariki na magharibi mwa nchi ili kufanikisha shughuli zao za upanzi wakati huu wa msimu mfupi wa mvua.

kra

Hayo yalibainika kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jana Jumanne katika Ikulu ya Nairobi.

Wakati wa mkutano huo, ilibainika kuwa mipango kabambe imewekwa na utawala wa Kenya Kwanza kuhakikisha kutakuwa na mbolea ya kutosha itakayotolewa kwa wakulima wakati wa msimu mrefu wa mvua mwakani.

Serikali inasema kumekuwa na ongezeko la mavuno kote nchini tangu kuanzishwa kwa mpango wa utoaji mbolea ya bei nafuu kwa wakulima.

 

Website | + posts