Home Vipindi Mifugo saba walioibwa kaunti ya Marsabit wapatikana

Mifugo saba walioibwa kaunti ya Marsabit wapatikana

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Marsabit Patrick Mwakio, alisema polisi vile vile walipata mifugo 12 na kufikisha idadi ya mifugo waliopatikana kuwa 19, kati ya mifugo 25 walioibwa.

0
kra

Maafisa wa polisi wamepata bunduki mbili na mifugo saba walioibwa katika kaunti ya Marsabit .

Hii ni baada ya kikosi cha maafisa wa usalama kuwafuata watu wanaoshukiwa kuwa majangili kufuatia shambulizi katika eneo la Malgis kando ya barabara kuu ya kutoka Marsabit kuelekea Isiolo siku 11 zilizopita.

kra

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Marsabit Patrick Mwakio, alisema polisi vile vile walipata mifugo 12 na kufikisha idadi ya mifugo waliopatikana kuwa 19, kati ya mifugo 25 walioibwa.

Mwakio akisema hakuna majeruhi walioripotiwa wakati wa tukio hilo na kwamba msako wa majangili hao unaendelea.

Wakati wa tukio hilo, watu wanaoshukiwa kuwa majangili waliojihami walishambuliza lori lililokuwa likisafirisha mifugo 25 kuelekea Nairobi likiwa chini ya ulinzi wa maafisa wawili wa polisi.

Afisa mmoja wa polisi aliuawa huku mwenzake akipata majeraha mabaya ya risasi.

Mwakio aliwapongeza maafisa hao wa usalama kwa kujitolea kutekeleza jukumu lao akiongeza kuwa hawatalegea hadi mifugo waliosalia watakapopatikana na wahusika kuadhibiwa

Website | + posts