Home Habari Kuu Mifugo 229 walioibwa Baringo wapatikana

Mifugo 229 walioibwa Baringo wapatikana

Wakati wa oparesheni hiyo kulitokea ufyatulianaji risasi kati ya polisi na washukiwa hao lakini hakuna yeyote alijeruhiwa.

0
Mifugo walioibwa Baringo wapatikana

Mifugo 229 walioibwa na majangili katika eneo la Barchar, kaunti ya Baringo, wamepatikana na kurejeshewa wenyewe.

Kupitia kwa taarifa, huduma ya taifa ya polisi, ilisema msako wa pamoja uliojumuisha maafisa wa polisi kutoka kikosi maalum, polisi wa kawaida na wale wa akiba, walichukua hatua za haraka kuwatafuta mifugo hao na kuwapata.

Wakati wa oparesheni hiyo kulitokea ufyatulianaji risasi kati ya polisi na washukiwa hao lakini hakuna yeyote alijeruhiwa.

“Kulikuwa na makabiliano ya risasi kati ya maafisa hao wa usalama na majangili, lakini hakuna majeruhi walioripotiwa,” ilisema huduma ya taifa ya polisi.

Aidha huduma ya taifa ya polisi ilielezea kujitolea kwake kukabiliana na visa vya ujangili.

Idara ya polisi imekariri kujitolea kwake kukabiliana na ujangili.

Website | + posts