Home Habari Kuu Michezo ya Olimpiki yafunguliwa kwa sherehe za kufana Paris

Michezo ya Olimpiki yafunguliwa kwa sherehe za kufana Paris

0
kra

Nahodha wa timu ya taifa ya Voliboli ya Kenya kwa vipusa Triza Atuka na mshikilizi wa rekodi ya Afrika ya mita 100, Ferdinand Omanyala waliongoza timu ya  Kenya, katika sherehe za kufungua rasmi makala ya 33 ya Michezo Olimpiki jijini Paris Ufaransa Ijumaa usiku.

Zaidi ya mataifa 200 yalishriki hafla hiy,o iliyoandaliwa katika mto Seine katikati ya jiji  Paris kwa mara ya kwanza ,kinyume na awali ambapo sherehe za ufunguzi zimeandaliwa ndani ya uwanja .

kra

Kikosi cha Kenya katika sherehe hizo kilivalia sare rasmi nyekundu za ulimbwende wa Kimaasai kikipiga gwaride kwa kutumia meli.

Wanariadha zaidi ya 7,000 walipiga gwaride wakati wa sherehe hizo wakitumia mashua na meli zaidi ya 80, zilizozunguka umbali wa kilomita sita katika mto wa Seine.

Mchezaji soka wa mstaafu wa Ufaransa Zinedine Zidane alibeba mwenge wa olimpiki,  katika sherehe hiyo iliyoanza mida saa mbili unusu usiku na kuchukua takriban saa tatu unusu.

Zaidi ya mashabiki laki tatu walisimama juu ya daraja za mto huo ,nje ya majumba yao ya orofa,roshani na juu ya meli kutazama tafrija hiyo adimu na ya kipekee.

Bendera ya Olimpiki  ilipandishwa rasmi juu ya mnara wa maarufu wa Eiffel Tower jijini Paris.

Wasanii maarufu , Aya Nakamura, Lady Gaga na Celine Dion walitumbuiza umati wa watu kwa vibao vyao maridhawa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alifungua rasmi michezo hiyo iliyo na kaulimbiu ya ‘Games wide open’.

Mashindano hayo yaliyoanza Julai 24 kwa fani za raga ya wanaume saba upande na kandanda, yataanza rasmi Jumamosi hii ikiwa siku ya kwanza baada ya kufunguliwa.

Kenya inawakilishwa na wanamicehzo 81 wanaoshiriki fani sita za Judo,raga,uogleaji,fencing,voliboli na riadha.