Michezo ya Olimpiki kwa wanamichezo walemavu itafungwa rasmi Jumapili usiku, baada ya kudumu kwa zaidi ya majuma mawili.
Olimpiki kwa walemavu ilishirikisha zaidi ya nchi 100, huku 73 pekee zikishinda madali.
Sherehe za kufunga michezo hiyo zitaandaliwa Jumapili na kupeperushwa mubasahara na runinga ya taifa,KBC Channel 1.
China ilimaliza ya kwanza kwenye msimamo wa nishani kwa medali 220,dhahabu 94 ,fedha 76 na shaba 50.
Uingereza ilifuatia katika nafasi ya pili kwa dhahabu 49,fedha 44 na shaba 31,wakati Marekani ikimaliza ya tatu, kwa dhahabu 36 fedha 42 na shaba 27.
Kenya ilimaliza ya 75 kwa nishani moja pekee ya fedha iliyoshindwa na Samson Ojuka katika shindano la kuruka mapana.