Home Kimataifa Mhubiri Paul Mackenzie kusalia kizuizini kwa siku 47 zaidi

Mhubiri Paul Mackenzie kusalia kizuizini kwa siku 47 zaidi

0
Self-proclaimed pastor Paul Nthenge Mackenzie, who set up the Good News International Church in 2003 and is accused of inciting cult followers to starve to death "to meet Jesus", appears in the dock at the court in Malindi on May 2, 2023. - A Kenyan pastor appearing in court on May 2, 2023 will face terrorism charges, prosecutors said in connection with the deaths of over 100 people found buried in what has been dubbed the "Shakahola forest massacre". The deeply religious Christian-majority country has been stunned by the discovery of mass graves last month in a forest near the Indian Ocean coastal town of Malindi. (Photo by SIMON MAINA / AFP)
kra

Mhubiri tata Paul Mackenzie ataendelea kuramba maisha ya kizuizini kwa siku zingine 47 baada ya mahakama moja ya Shanzu kuwaruhusu polisi kuendelea kumzuilia. 

Hakimu Mkuu wa mahakama ya Shanzu Yusuf Shikanda alielekeza kwamba Mackenzie pamoja na washtakiwa wengine wenza 28 wasalie kizuizini kwa kipindi cha siku zingine 47 ili kuruhusu kukamilishwa kwa uchunguzi.

kra

Mackenzie amekuwa kizuizini kwa siku 90 zilizopita.

Agosti 2, 2023, kiongozi wa mashtaka alitaka polisi wakubaliwe kuendelea kuwazuilia washukiwa hao kwa wiki zisizopungua saba ili kuruhusu kukamilishwa kwa uchunguzi.

Hii ni kutokana na kuthibitishwa kwa vifo zaidi ya 400 katika msitu wa Shakahola, vifo anavyohusishwa navyo Mackenzie ambaye ni mhubiri wa dhehebu la Good News  International. Mhubiri huyo anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Mackenzie, mkewe Rhoda Maweu na washtakiwa wenza wanakabiliwa na zaidi ya mashtaka 21 ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki.

 

Martin Mwanje & Haniel Mengistu
+ posts