Home Kimataifa Mhubiri Ezekiel bado hajaponyoka!

Mhubiri Ezekiel bado hajaponyoka!

0
kra

Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma nchini DPP imefafanua kwamba Mhubiri Ezekiel Odero wa kanisa la New Life Prayer center bado hajaondolewa mashtkata.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, afisi hiyo ilifafanua kwamba faili iliyofungwa na mahakama ya Shanzu ni ya kumzuilia mhubiri huyo lakini ile ya kumchunguza bado iko wazi na anaendelea kuchunguzwa.

kra

Taarifa hiyo inaelezea kwamba awali afisi hiyo ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ilikuwa imeomba mahakama kwamba mhubiri huyo azuiliwe kwa siku 30 kutoa fursa kwa uchunguzi, lakini akaachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 1.5 na masharti kwamba asiingilie mashahidi kwa vyovyote na awe akiripoti kwa wachunguzi wa kesi hiyo kila wiki.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma atatoa mwongozo wa hatua itakayofuata baada ya kudurusu faili ya uchunguzi wa kesi dhidi ya Odero.

Odero alikamatwa na maafisa wa polisi kwa kudhaniwa kuwa na uhusiano na mhubiri tata Paul Mackenzie ambaye yuko kizuizini na ambaye anahusishwa na vifo vya watu wengi katika msitu wa Shakahola.

Waliookolewa kutoka kwenye msitu huo ambao walikiri kuwa wafuasi wa Mackenzie walielezea kwamba aliwaelekeza wafunge kula na kunywa ili waweze kumwona Yesu.

Website | + posts