Home Habari Kuu Mhubiri David Gakuyo kufikishwa kizimbani Alhamisi

Mhubiri David Gakuyo kufikishwa kizimbani Alhamisi

0

Mhubiri wa runinga David Kariuki Ngari maarufu kama Gakuyo, anatarajiwa kuwasilishwa mahakamani siku ya Alhamisi Februari 22, baada ya kukesha korokoroni Jumatano usiku kwa kosa la wizi.

Gakuyo anakabiliwa na makosa ya wizi wa shilingi bilioni 1.3 za wanachama wa shirika la mikopo na akiba la Ekeza.

Mhubiri huyo alikamatwa na maafisa polisi katika angatua ya kimataifa ya Jomo Kenyatta akisafiri kuelekea nchini Zambia kwa shughuli za kibiashara.

Gakuo alipelekwa hadi makao makuu ya DCI Jumatano usiku punde baada ya kutiwa mbaroni, alipohojiwa kwa masaa kadhaa kabla ya kupelekwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga alipokesha.

Majasusi wanapendekeza Gakuyo azuiliwe kwa muda zaidi wakisubiri idhini ya kuondolewa kwa mashtaka yote kutoka lwa afisi ya Mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Hata hivyo kulingana na wakili wake Ndegwa Njiru, mhubiri huyo alikubaliana na waliokuwa wanamdai na kuwarejeshea pesa zao zote na hivyo alikamatwa kimakosa na polisi.