Home Kaunti Mgonjwa wa kwanza kuambukizwa Mpox nchini Kenya amepona

Mgonjwa wa kwanza kuambukizwa Mpox nchini Kenya amepona

Muthoni alisema ufuatiliaji wa wizara hiyo umeimarishwa katika maeneo ya mpakani.

0
kra

Mgonjwa wa kwanza ambaye aliambukizwa ugonjwa wa Mpox hapa nchini amepona, imesema Wizara ya Afya.

Kupitia kwa taarifa iliyotolewa Jumanne alasiri na katibu katika wizara ya afya anayehusika na maswala ya afya ya  umma Mary Muthoni, mgonjwa huyo amekuwa akichunguzwa kwa karibu na kutibiwa na maafisa wa wizara wanaochunguza kisa hicho na kiwango chake cha maambukizi.

kra

Akizungumza katika makao makuu ya Wizara ya Afya jijini Nairobi, Muthoni alisema ufuatiliaji wa wizara hiyo umeimarishwa katika maeneo ya mpakani.

“Kutokana na maambukizi ya MPOX na kuambatana na miongozo ya kimataifa ya kukabiliana na ugonjwa huo, wizara ya afya idara ya afya ya serikali ya kauntinya Taita Taveta ziliaza kuwatambua wale wote walikaribiana na mgonjwa huyo kazini, hospitalini na njiani alikopitia akiwa safarini,” alisema katibu Muthoni.

Muthoni alisema wizara hiyo imeweka mikakati kadhaa ya  kuzingatiwa ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Website | + posts