Home Kaunti Mgomo wa wahudumu wa afya Meru waendelea

Mgomo wa wahudumu wa afya Meru waendelea

0
kra

Mgomo wa wahudumu wa afya katika kaunti ya Meru unaendelea leo ikiwa siku ya sita na umesababisha tatizo kubwa katika sekta ya afya kwenye kaunti hiyo huku huduma zikilemazwa katika vituo mbali mbali vya afya vya serikali.

Wahudumu hao waliandamana leo hadi afisi za serikali ya kaunti ya Meru kufuatia malalamishi yao yanayojumuisha uchache wa walioajiriwa, kukosa kupandishwa vyeo na mengine.

kra

Walisema madaktari 144 walioajiriwa na serikali ya kaunti ya Meru na wahudumu wengine wa sekta ya afya wameghadhabishwa na hatua ya serikali ya kaunti ya kukosa kutekeleza makubaliano ya pamoja yaliyoafikiwa Oktoba 6, 2023.

Inaripotiwa kwamba maafisa wakuu wa chama cha madaktari nchini na wawakilishi wa serikali ya Meru walikubaliana wakati huo kwamba bodi ya utumishi wa umma ya kaunti hiyo iajiri madaktari katika kiwango cha M-N kufikia Novemba 2023.

Utekelezaji wa kupandishwa vyeo kwa madaktari katika malipo ulistahili kuanza Aprili Mosi 2024 ambapo pia wangelipwa pesa zote za awali, hatua ambayo haijachukuliwa hadi sasa.

Katibu wa tawi la Meru la chama cha maafisa tabibu nchini Kenya Union of Clinical Officers – KUCO Moses Baiyenia amesema kwamba suala kuu kati ya malalamishi yao ni kupandishwa vyeo.

Website | + posts
Jeff Mwangi
+ posts