Home Habari Kuu Mgomo ungalipo: Madaktari wasimama kidete licha ya kikao na Waziri Nakhumicha

Mgomo ungalipo: Madaktari wasimama kidete licha ya kikao na Waziri Nakhumicha

0

Chama cha madaktari nchni, KMPDU kimekanusha madai ya kuafikia makubaliano na serikali na kusisitiza kuendelea na mgomo wao wa kitaifa ambao umeingia siku ya tano leo Jumatatu.

Wakizungumza na wanahabari, viongozi wa KMPDU wamesema  licha ya kufanya mkutano na Wizara ya Afya, hawakuafikia suluhu yoyote na kuapa kuendelea kususia kazi.

Matamshi ya KMPDU yanajiri muda mfupi baada ya waziri wa Afya Susan Nakhumicha kutangaza kuwa serikali itaanza kuwatuma madaktari wanagenzi kwa vituo vya afya kuanzia Aprili mosi.

Huduma za afya  zimelemazwa katika hospitali zote za umma nchini tangu kuanza kwa mgomo huo wa madaktari, hali ambayo imewatatiza wagonjwa wengi wanaolazimika kutafuta huduma za matibabu katika hospotali za kibinafsi.

Website | + posts