Home Kimataifa Mganga bandia akamatwa Tanzania

Mganga bandia akamatwa Tanzania

0

Maafisa wa polisi nchini Tanzania hususan mkoani Dar es salaam, wamemkamata jamaa kwa jina Lucas Salumu Baswege wa umri wa miaka 42 aliyejisingizia kuwa mganga.

Mkazi huyo wa eneo la Kisemvule, Mkuranga anatuhumiwa kwa kuwapa kileo zaidi ya watu 16 katika maeneo tofauti kabla ya kuwaibia.

Kamanda wa polisi wa kanda ya Dar es salaam Muliro Jumanne ameelezea kwamba mshukiwa alitekeleza kitendo hicho katika maeneo kama Mjimwema Kigamboni, Tuangoma, Kilungule na Ubungo.

Mali ambayo aliibia watu kama pikipiki na simu 10 za rununu tayari imetambuliwa na wamiliki.

Polisi walimkamata pia Thomas Mhagama wa umri wa miaka 35 ambaye ni fundi wa simu kwa tuhuma za kushirikiana na mganga huyo bandia. Amekuwa akipata simu zilizoibwa kutoka kwa Baswege na kisha kuuzia wateja.

Washukiwa hao watafikishwa mahakamani Dar es Salaam.

Website | + posts