Home Kaunti Mfugaji auawa, wawili wajeruhiwa kaunti ya Meru

Mfugaji auawa, wawili wajeruhiwa kaunti ya Meru

Naibu wa kamishna alisema kisa hicho ni cha tatu mwezi huu,

Mfugaji mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi huku wengine wawili wakijeruhiwa baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wezi wa mifugo kuvamia kijiji cha Ngachiru,kaunti ndogo ya Igembe kaskazini kaunti ya Meru.

Kulingana na naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Igembe Kaskazini Silvester Manguru, idadi isiyojulikana ya washambulizi wanaoaminika kutoka kaunti jirani ya Isiolo na waliokuwa wamejihami na silaha, walivamia kijiji hicho Alhamisi jioni na kumpiga risasi mfugaji huyo na kuwajeruhi wengine wawili kabla ya kutoroka na idadi isiyojulikana ya ng’ombe na mbuzi.

Manguru alisema wawili waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Mutuati, huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika chumba cha wafu katika hospitali ya Maua.

Aidha naibu huyo wa kamishna alisema kisa hicho ni cha tatu mwezi huu, huku akiwasihi wakazi kuwa watulivu huku maafisa wa polisi wakiwatafuta majangili hao.

Alihakikisha kuwa serikali haitawavumilia wahalifu, akionya kuwa watakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria.

Website | + posts
Jeff Mwangi
+ posts