Home Habari Kuu Mfanyakazi wa serikali ya kaunti ya Mombasa akamatwa kwa kuitisha hongo

Mfanyakazi wa serikali ya kaunti ya Mombasa akamatwa kwa kuitisha hongo

0

Mfanyakazi mmoja wa serikali ya kaunti ya Mombasa amekamatwa kwa tuhuma za kuitisha hongo. 

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC katika taarifa inasema imemkamata  Tarim Abdul Karim kwa madai ya kuitisha hongo ya shilingi 15,000 kutoka kwa raia.

Karim alitaka apewe fedha hizo kama sharti la kumkabidhi raia huyo leseni.

Kulingana na EACC, mshukiwa alikamatwa jana Jumatano na kupelekwa katika Ofisi ya Kanda ya Pwani ya tume hiyo mjini Mombasa na kwamba atafikishwa mahakamani punde baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

Tume hiyo imewapongeza Wakenya kwa kuwa mstari wa mbele kuripoti visa vya uitishaji hongo katika vituo ya utoaji huduma.

Imewataka Wakenya kuendelea kufanya hivyo kupitia nambari isiyotozwa malipo ya 1551.

Website | + posts