Home Kimataifa Mfanyakazi aokolewa siku tano baada ya jengo kuporomoka Afrika Kusini

Mfanyakazi aokolewa siku tano baada ya jengo kuporomoka Afrika Kusini

Kiongozi wa jimbo la Western Cape Alan Winde amesema kwamba uokoaji huo ulikuwa muujiza waliokuwa wakiutarajia.

0
Jengo lililoporomoka Afrika Kusini.
kiico

Mfanyakazi ameokolewa kwenye vifusi vya jumba lililoporomoka katika mji wa George Afrika Kusini, baada ya kukwama kwa siku tano.

Waokoaji walifanikiwa kuwasiliana na mwanamume huyo na kumpa maji ya kunywa baada ya kumsikia akiwa chini ya vifusi.

Kiongozi wa jimbo la Western Cape Alan Winde amesema kwamba uokoaji huo ulikuwa muujiza waliokuwa wakiutarajia.

Jumba hilo ambalo lilikuwa limekamilika ujenzi kwa upande mmoja huku mwingine ukiendelea kujengwa, uliporomoka Jumatatu na kusababisha vifo vya watu 14 huku wengine 39 wakiwa hawajulikani waliko.

Watu 81 walikuwa wakifanya kazi kwenye mjengo huo wakati wa ajali hiyo, kwa mujibu wa taarifa ya usimamizi wa mji huo, ambapo 13 ya waliookolewa wanapokea matibabu hospitalini.

Uokoaji wa hivi punde unafuatia mwingine wa Delvin Safels mwenye umri wa miaka 29 aliyeondolewa kwenye vifusi Jumatano Mei 8 .

Uokozi wake uliwavutia wengi baada ya yeye kuwatumia familia yake ujumbe wa sauti mara kwa mara kwamba anawapenda na akiwa mwenye hofu kwamba hataokolewa.

kiico