Mshukiwa mkuu wa sakata ya mafuta ya Triton yenye thamani ya shilingi bilioni 7.6 Yagnesh Devani ameachiliwa kwa dhamana.
Bilionea Devani ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 20 na mdhamini wa kiasi kama hicho au shilingi milioni 5 pesa taslimu.
Mshukiwa huyo alikamatwa Agosti 6, 2024 na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC kuhusiana na sakata hiyo ya mwaka wa 2008.
EACC ilimkamata Devani akiwa kwenye ofisi zake jijini Nairobi. na hivyo kusitisha juhudi zake za muda mrefu za kukwepa mkono wa sheria baada ya kuwa mafichoni.
Agizo la mahakama la kukamatwa kwake lilikuwa limetolewa mnamo mwaka wa 2009.