Home Burudani Mfahamu mwamamuziki Pepe Kale

Mfahamu mwamamuziki Pepe Kale

0

Kwa muda mrefu hasa barani Afrika,muziki wa rumba kutoka DRC umevuma kutokana na ladha na miondoko ya wanamitindo wake k.v.

Pepe Kalle, François Luambo Luanzo Makiadi, Madilu System na wengine.

Wanamuziki hawa wanajulikana hata kwa vizazi vya sasa kwani bado miziki yao ina mashiko makubwa.

Kwenye maka ya mwanga wa wiki hii leo, tunamwangazia Pepe Kalle a.k.a Tembo wa Afrika.

Pepe Kalle alizaliwa namo tarehe 30 desemba 1951 mjini Kinshasa wakati huo ukiitwa Leopold kutokana ukoloni wa wabelgiji.

Alipewa jina Jean Kabasele Yampanya na alikuwa na urefu futi sita na ncha 11 huku uzani wake ukiwa kilo 150.

Alianza muziki katika bendi ya Afrikan Jazz kisha akahamia Bella Bella na Lipua lipua.

Namo mwaka wa 1972, yeye na wenzake Diludilumona na Papy tex, waliondoka Lipua lipua na kuunda bendi yao ya ‘’Empire Bakuba” jina lililotokana na kundi na kivita nchini humo

Walilenga kutumia midundo iliyopuuzwa kutoka mashinani mwa DRC wakati huo ikiitwa zaire chini ya rais Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa za Banga.

Bendi yao ilivuma kwa haraka walipotoa vibao motomoto k.v. dadou na sango ya mawa, wakitumia miondoko ya Kwasa Kwasa iliyotikisa Kinshasa.

Hatua hii ilipekea kushinda kura ya bendi bora namo mwaka wa 1982 wakati wakiaadhimisha miaka 10 ya bendi hiyo.

Pepe kalle na kundi lake walizidi kuimba na kutamba nchini humo na Afrika magharibi.

Mwaka wa 1986, alifanya ushirikiano na Nyomba na kutoa album ya Zouke Zouke iliyoleta mapato mengi.

Namo mwaka wa 1988, alitetemesha Afrika na wimbo Moyibi (bakule bakule).

Pepe kalle vile vile alifuatilia kwa karibu sifa za mwana soka maarufu wa Cameroon Roger Milla na kumzawadi wimbo maalum menye kasi na mtindo wa Soukous uliorekodiwa ufaranza.

Kutokana na mapenzi yake kwa walemavu, Kalle alijumuisha Jollie Bebe, Dominic Mabwa na Ayilla Emoro kwenye bendi ila haikukujukua muda kabla ya Emoro kufariki wakiwa nchini Botswana.

Kifo hiki kilimguza mshipa Kalle hadi kupelekea bendi yake kutunga wimbo wa kumkumbuka Emoro uitwao Mabele riche.

Licha ya hayo, aliendelea kubuni albamu zingine kama Gigantic afrique, larger than life na cock tail. Tena alishirikiana na gwiji Lutumba Simaro Massiya na N’yoka Longo.

Maisha ya kjamii.

Alikuwa mzalendo licha ya ugumu wa maisha uliosababishwa na utawala wa rais Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa za Banga.

Alifanya patanisho na vigogo kama Tabuley na mwahabari Achilles Ngolie ambaye aliangazia bendi hiyo mno katika kazi yake.

Ametajwa kuwa na akili kama ya ndovu kwani alielewa na kukumbuka mambo mengi kwa ufasaha.

Familia.

Alioa Pauline Lundokisi na walijaaliwa watoto watano. Pauline alifariki dunia 2019.

Kifo.

Alifariki dunia mapema mwa tarehe 29 Nov.1998 akiwa hospitalini jijini Kinshasa kutokana na mshtuko wa moyo.

Alipewa mazishi ya kitaifa na mwili wake kutembezwa jijini Kinshasa kwa heshima za mwisho kutoka kwa mamilioni ya wafuasi wake.

Alizikwa kwenye makaburi ya Gombe tarehe 6 Dec.1998.