Home Habari Kuu Mfahamu Mkuu wa vikosi vya ulinzi aliyefariki Jenerali Francis Ogolla

Mfahamu Mkuu wa vikosi vya ulinzi aliyefariki Jenerali Francis Ogolla

Rais William Ruto alimpandisha cheo Luteni Jenerali Francis Ogolla kuwa Jenerali Aprili 28, 2023, kabla ya kumteua kuwa mkuu wa vikosi vya ulinzi Aprili 29, 2023.

0
Mkuu wa vikosi vya ulinzi aliyefariki Jenerali Francis Ogolla.

Jenerali Francis Omondi Ogolla alijinga na vikosi vya ulinzi KDF Aprili 24 1984, na kisha akateuliwa Luteni wa pili Mei, 6, 1985 na kujiunga na jeshi la wanahewa.

Alipohudumu katika vikosi vya ulinzi nchini KDF, Jenerali Ogolla alishikilia nyadhifa kadhaa, zikiwa ni pamoja na mkufunzi katika chuo cha mafunzo ya ndege za kijeshi, kamanda wa kambi ya Laikipia ya jeshi la wanahewa na naibu kamanda wa jeshi la wanahewa.

Rais William Ruto alimpandisha cheo Luteni Jenerali Francis Ogolla kuwa Jenerali Aprili 28, 2023, kabla ya kumteua kuwa mkuu wa vikosi vya ulinzi Aprili 29, 2023.

Jenerali Ogolla alisomea maswala kadhaa ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya rubani wa ndege aina ya USAF, mafunzo ya ujasusi, kukabiliana na ugaidi na uchunguzi wa ajali.

Jenerali Francis Ogolla ana stashahada katika masomo ya Kimataifa na Sayansi ya Kijeshi katika chuo Kikuu cha Egerton, Shahada ya Sanaa katika Sayansi ya Siasa, Migogoro ya Silaha na mafunzo ya amani na Shahada ya Uzamili ya sanaa katika Mafunzo ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

Aidha alihudumu wadhifa wa mwenyekiti wa ushirika wa kijeshi wa Kikristo kuanzia mwaka 1994 hadi 2004 na Mwenyekiti mwenza wa Chama cha Wakuu wa wanajeshi wa angani wa Afrika kati ya 2018-2019.

Website | + posts