Home Burudani Meta yaunda mtandao sawia na Twitter

Meta yaunda mtandao sawia na Twitter

0
kra

Meta kampuni inayomiliki mitandao ya kijamii kama vile Facebook, WhatsApp, na Instagram, imezindua mtandao mpya utakaoshindana na Twitter.

Mtandao huo unaoitwa Threads, utazinduliwa rasmi Alhamisi Julai 6, 2023 na utaunganishwa na Instagram.

kra

Kulingana na Meta jukwaa hilo jipya kwenye mitandao ya kijamii litatoa fursa kwa watumiaji kuzungumzia kwa kina matukio ya sasa na yanayotarajiwa.

Wengi wanachukulia hatua ya Meta kama ushindani ikizingatiwa kwamba watumiaji wa Twitter wamekuwa wakipokea masharti mapya. Sharti la hivi karibuni zaidi ni kiwango cha jumbe ambazo kila mtumiaji anaweza kuona na kusoma.

Haya yanajiri siku chache baada ya mmiliki wa Meta Mark Zuckerberg na mmiliki wa Twitter Elon Musk kutangaza kwamba watapigana kizimbani. Huenda haya ndiyo mashindano wawili hao walikuwa wanazungumzia.

Meta inaelezea kwamba Threads ni jukwaa la kutumiana jumbe ambapo jamii inaweza kuzungumza kuhusu mambo mengi tofauti, ya sasa na yajayo.