Home Kimataifa Meli za kivita za Urusi zawasili China

Meli za kivita za Urusi zawasili China

0

Meli mbili kubwa za kivita za Urusi zimewasili mjini Shanghai, China kwa ziara ya kwanza ya bandari ya meli hizo nchini China katika muda wa miaka mitatu. Ujio huo ni dhihirisho jingine la ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili, miezi 16 baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Meli hizo za enzi ya vita baridi ziitwazo “Gromkiy” na “Sovershenniy” ziliwasili katika jiji kubwa kabisa la China jana Jumatano na kukaribishwa na gwaride la mabaharia wa Uchina waliokuwa wamevaa sare ya rangi nyeupe. Mabaharia hao walikuwa wamebeba mabango yenye maneno ya kukaribisha meli hizo kwa mujibu wa shirika la habari la TASS.

Meli hizo ambazo kawaida huegeshwa huko Vladivostok, zitasalia China hadi Julai 11, 2023 na zinatarajiwa kutumika katika mafunzo kwa wanamaji wa nchi hizo mbili wakiangazia mawasiliano kutoka kwa meli moja hadi nyingine, ujanja wa kukwepa adui baharini na mbinu za kutafuta na kuokoa watu kutoka kwenye maji.

Mwakilishi wa kamati ya mambo ya nje ya China Dmitry Lukyantsev alisema ujio wa meli hizo za kivita za Urusi ni muhimu na ndiyo mara ya kwanza meli za Pasifiki zinatumika baada ya kipindi cha miaka mitatu cha janga la virusi vya korona.

Aliongeza kwamba hatua hiyo inaonyesha ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili umedumishwa katika nyanja zote kama vile ulinzi na siasa.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here