Home Kimataifa Meli ya kubeba mafuta yashambuliwa katika pwani ya Yemen

Meli ya kubeba mafuta yashambuliwa katika pwani ya Yemen

Waasi wa Houthi wamedai kutekeleza shambulio hilo.

0
Meli ya kubeba mafuta yashambuliwa katika Pwani ya Yemen.

Meli ya mafuta ghafi imeharibiwa katika shambulio la kombora katika pwani ya Yemen -shambulio wa hivi punde zaidi kufanywa na waasi wa kihouthi.

Tukio hilo lilitokea maili 15 kusini-magharibi mwa mji wa Mocha nchini Yemen.

Shirika la usalama wa baharini la Uingereza UKMTO liliripoti kuwa meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Panama ilipigwa mara mbili na imeharibiwa.

Hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa na tukio hilo linachunguzwa.

Kulingana na UKMTO, shambulio la kwanza la kombora lilisababisha mlipuko karibu na meli na kuhisiwa na waliokuwa ndani. Ya pili – iliyofikiriwa kuhusisha makombora mawili – iliwasiliana.

Kampuni ya kimataifa ya kudhibiti hatari ya Ambrey ilisema kuwa makombora matatu yameonekana.

Imeongeza kuwa makombora ya balistiki yameripotiwa kurushwa kutoka kwa jimbo la kusini-magharibi la Taiz nchini Yemen.

Waasi wa Houthi wamedai kutekeleza shambulio hilo.

Msemaji wa jeshi la kundi hilo, Yahya Sarea, alisema katika hotuba yake Jumamosi kwamba meli ya “Uingereza” iitwayo Andromeda Star ilikuwa ikilengwa, katika hali iliyosababisha “shambulio la moja kwa moja”.

Kamandi Kuu ya Marekani ilithibitisha kwamba Andromeda Star ndiyo meli inayozungumziwa, kwamba imepata uharibifu mdogo na inaendelea na safari yake.

Ambrey aliripoti kwamba meli ya mafuta iliyoshambuliwa ilikuwa inamilikiwa na Uingereza hadi Novemba 2023.

Mmiliki wake wa sasa amesajiliwa Ushelisheli na meli hiyo imekuwa akijishughulisha na biashara inayohusishwa na Urusi – ikisafiri kutoka mjini Primorsk nchini Urusi hadi Vadinar, katika jimbo la India la Gujarat, wakati shambulio hilo lilipotokea.

Ambrey alishauri wamiliki wa meli na waendeshaji kufanya “ukaguzi wa kina wa uhusiano” kabla ya kuvuka eneo hilo “kwani Wahouthi wanaweza kuhusisha meli na mmiliki wa kizamani”.