Home Michezo Mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika kutifua vumbi Ijumaa

Mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika kutifua vumbi Ijumaa

0
Karidioula Tresor Mofosse of Asec Mimosa celebrates goal with teammates during the 2023/24 CAF Champions League 2nd leg qualification match between ASEC Mimosas and Al Ahly Benghazi in Bouake Stadium, Bouake, Côte d'Ivoire on 1 October 2023 ©BackpagePix

Michuano ya makundi kuwania kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza Ijumaa Pyramids ya Misri ikiwaalika mabingwa mara tano TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kundi A.

Mabingwa wa Algeria CR Belouizdad watamenyana na Young Africans SC ya Tanzania Ijumaa usiku katika kundi D.

Katika kundi B Jumamosi, Simba SC itawaalika miamba wa Ivory Coast Asec Mimmosas.

Petro Atletico ya Angola itakuwa mwenyeji wa Al Hilal ya Sudan katika mechi ya kundi C Jumamosi.

Katika kundi C, Etoile Sahel watakuwa ziarani dhidi ya wenzao Esperance huku mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri ikiwaalika Medeama ya Ghana kesho Jumamosi katika mechi ya kundi D.

Wydad Casablanca ya Morocco itafungua msimu dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana katika kundi B kesho Jumamosi kisha Mamelodi Sundowns wawe nyumbani Jumapili dhidi ya FC Nouadhibou kutoka Mauritania kundini A.

Kundi A: Mamelodi Sundowns (South Africa), Pyramids FC (Egypt), TP Mazembe (DRC), FC Nouadhibou (Mauritania)

Kundi B: Wydad AC (Morocco), Simba SC (Tanzania), Asec Mimosas (Cote d’Ivoire), Jwaneng Galaxy (Botswana)

Kundi C: Esperance (Tunisia), Atletico Petroleos (Angola), Al Hilal (Sudan), Etoile du Sahel (Tunisia)

Kundi D: Al Ahly (Egypt), CR Belouizdad (Algeria), Young Africans (Tanzania), Medeama (Ghana)

Website | + posts