Home Kimataifa Mchungaji Joel Kandie achaguliwa mwenyekiti wa COTU

Mchungaji Joel Kandie achaguliwa mwenyekiti wa COTU

Chebii alichaguliwa wakati wa mkutano wa 111 wa bodi ya usimamizi wa COTU, ambapo pia Wycliffe Nyamwatta alichaguliwa naibu wa pili mwenyekiti wa COTU.

0
Mchungaji Joel Kandie Chebii.
kra

Bodi ya Muungano wa vyama vya wafanyikazi hapa nchini COTU, imemchagua mchungaji Joel Kandie Chebii kuwa mwenyekiti wake.

Kupitia kwa taarifa siku ya Ijumaa, katibu mkuu wa  COTU Francis Atwoli, alisema Chebii amehudumu katika muungano wa COTU kwa zaidi ya miongo minne na sasa anashikilia wadhifa wa katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi cha Tiles and Textile.

kra

Chebii alichaguliwa wakati wa mkutano wa 111 wa bodi ya usimamizi wa COTU, ambapo pia Wycliffe Nyamwatta alichaguliwa naibu wa pili mwenyekiti wa COTU.

Nyamwatta amekuwa mwanachama wa bodi ya COTU kwa muda wa miongo miwili na anashikilia wadhifa wa katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi cha Kenya Engineering.

Atwoli aliwahimiza viongozi hao walioachaguliwa kuendelea kuimarisha haki na masilahi ya wafanyakazi wa Kenya.

“Udhabiti ni nguzo muhimu katika shirika lolote, muungano wa COTU utaendelea kuhakikisha unadumisha umoja naudhabiti ili kuwahudumia wafanyakazi wa Kenya,”  alisema Atwoli.

Website | + posts