Home Burudani Mchekeshaji asimulia jinsi mkubwa wake kazini alijaribu kuzuia asiolewe

Mchekeshaji asimulia jinsi mkubwa wake kazini alijaribu kuzuia asiolewe

0

Hellen Paul ni mchekeshaji, mwigizaji na mtangazaji wa vipindi vya runinga nchini Nigeria na ameshangaza wengi baada ya kusimulia kuhusu alichofanyiwa na mkubwa wake.

Alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha mitandaoni kwa jina “The Honest Bunch Podcast” ambacho kinaongozwa na mwigizaji mwenza Chinedu Ani Emmanuel na wengine.

Bi. Hellen alisema kwamba alikuwa akifanya kazi na kampuni kwa jina TVC wakati huo akiwa kwenye mahusiano na Femi Bamisile ambaye sasa ni mume wake.

Anasema siku moja alimpeleka Femi kazini kwake na wakiwa huko, msimamizi wa masuala ya wafanyakazi akawaita na akauliza Femi, “Huyu ndiye mwanamke ambaye ungependa kuoa? Labda ujifurahishe tu naye lakini huyu hastahili kuwa mke.”

Alimshauri Femi atafute mwanamke wa hadhi yake kwani alikuwa wakili tajika, mwenye sura nzuri na ambaye alikuwa anajua kuvaa vizuri.

Ushauri huo kutoka kwa mtu ambaye Hellen alimtizamia kama baba ulimvunja moyo sana lakini Femi hakubadili mawazo kumhusu.

Femi na Hellen walifunga ndoa mwaka 2010 na wamebarikiwa na watoto wawili.

Hellen ambaye sasa ni mkufunzi wa chuo kikuu nchini Marekani, amekuwa akisimulia historia ya maisha yake ambapo alielezea kwamba alizaliwa kutokana na kisa cha ubakaji, akalelewa na nyanyake na alisikia watu wakimuita mwanaharamu.

Alisema dada za mamake walikuwa wanambagua sana walipokuwa wanazuru mama yao. Wakati mmoja walimpa mama pesa wakamwelekeza azitumie kujikimu na wala sio kuhudhumia mwanaharamu.

Website | + posts