Mbunge wa zamani Nandi Alfred Keter ametekwa nyara Jumapili adhuhuri na watu wasiojulikana mtaani Kileleshwa akitoka kwenye ibada.
Keter alikuwa kwenye gari lake la V8 akitoka kwenye ibada mtaani Kileleshwa, alipokamatwa na kutolewa kwenye gari lake na kuingizwa katika gari la Land Cruiser lililokuwa karibu.
Mbunge huyo wa zamani amesema kupitia mtandao wake wa kijamii kuwa alitekwa nyara na kupelekwa mahali pasipojulikana.
Kiini cha utekaji nyara huo na wahusika hakijabainika.