Home Kimataifa Mbunge wa Molo asamehe waliovamia makazi yake

Mbunge wa Molo asamehe waliovamia makazi yake

0
kra

Mbunge wa eneo la Molo kaunti ya Nakuru imani Kuria ametangaza kwamba amewasamehe wote ambao walivamia makazi yake na kusababisha uharibifu mkubwa.

Akizungumza wakati wa ziara ya kimaendeleo katika eneo la Elburgon kwenye eneo bunge lake, Kimani alisema, “Hata mimi wale wote wamenifanyia madhara, siku ya leo nimewasamehea.”

kra

Katika video iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya mtandao wa X, mbunge huyo aliongeza kusema kwamba anaitaka idara ya upelelezi wa jinai DCI, iwaondolee lawama vijana waliokamatwa na kushtakiwa kuhusiana na uvamizi wa makazi yake.

Kuria anataka vijana hao waachiliwe ili warejelee kazi zao za kawaida huku akiwaonya kwamba wasiwahi rudia makosa hayo tena.

Kuria ambaye anahudumu kama mwenyekiti wa kamati ya bunge ya fedha na mipango ya kitaifa iliyoasisi mswada wa fedha wa mwaka 2024 alijipata pabaya punde baada ya kupitishwa kwa mswada huo wa fedha wa mwaka 2024 bungeni.

Jumanne Juni 25, vijana waliokuwa na ghadhabu walivamia makazi ya mbunge huyo katika eneo bunge lake ambapo wanasemekana kuiba mifugo na kuharibu nyumba na magari.

Hasara iliyotokana na tukio hilo ilikadiriwa kuwa kubwa.

Hata hivyo maandamano ya vijana wa Gen Z yalisababisha Rais William Ruto akose kutia saini mswada huo kuwa sheria nabadala yake akaurejesha bungeni na pendekezo la kuutupilia mbali kikamilifu.

Bunge tayari limetupilia mbali mswada huo.

Website | + posts