Home Habari Kuu Mbunge Peter Salasya atakiwa kufika mbele ya tume ya EACC

Mbunge Peter Salasya atakiwa kufika mbele ya tume ya EACC

Mbunge huyo anatarajiwa kufika katika afisi za tume hiyo Jumanne wiki ijayo kuandikisha taarifa.

0

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya ameagizwa kufika mbele ya tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC.

Mbunge huyo anatarajiwa kufika katika afisi za tume hiyo Jumanne wiki ijayo kuandikisha taarifa.

Salasya anamulikwa na tume ya EACC kwa madai ya kukiuka sura ya sita ya katiba kwa kumshambulia hadharani mwakilishi wadi ya Malaha-Isongo-Makunga Peter Walunya Indimuli wakati wa hafla ya mazishi katika eneo bunge la Mumias Mashariki kaunti ya Kakamega.

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya EACC Twalib Mbarak, amesema madai dhidi ya Salasya yanahusisha masuala muhimu ya kimaadili na endapo yatathibitishwa basi utakuwa ukiukaji mkubwa wa kanuni za maadili kwa afisa wa serikali.

Katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, mbunge huyo alionyeshwa akimshambulia mwakilishi wadi ya Malaha-Isongo-Makunga.

Website | + posts