Home Biashara Mbadi: Nitaimarisha uchumi wa taifa hili

Mbadi: Nitaimarisha uchumi wa taifa hili

Mbadi alisema atajizatiti kuona bidii yake inazaa matunda katika muda wa mwaka mmoja.

0
Waziri wa Fedha John Mbadi.
kra

Waziri wa fedha na mipango ya uchumi John Mbadi, amesema atajizatiti kuhakikisha uchumi wa taifa hili unaimarika.

Huku akimshukuru Rais William Ruto kumteua katika wadhifa huo, Mbadi alisema atajizatiti kuona bidii yake inazaa matunda katika muda wa mwaka mmoja.

kra

Akiongea Alhamisi wakati wa sherehe ya kutoa shukrani katika eneo la Suba Kusini, kaunti ya Homa Bay iliyohudhuriwa na Rais William Ruto, waziri huyo aliwataka wakenya kusahau siasa za kikabila na kukumbatia umoja hapa nchini.

“Sisi ni wa taifa moja liitwalo Kenya. Tusahau siasa za kikabila na utengano, na tuangazie maendeleo,” alisema Mbadi.

Kwa upende wake mwenyekiti wa chama cha Orange Democratic Movement Gladys Wanga, alisema chama hicho kinamkaribisha Rais Ruto katika eneo hilo, na wakati huo huo alipongeza ushirikiano uliopo kati ya Rais Ruto na Raila Odinga.

“Kama chama cha ODM, tunamkaribisha Rais Ruto katika eneo la Nyanza na pia ninamkaribisha kama Gavana wa kaunti ya Homa Bay,” alisema Wanga.

Viongozi waliozungumza katika hafla hiyo, walimshukuru Rais Ruto kwa kumchagua Mbadi kuwa waziri wa fedha, huku mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, akielezea imani yake kuwa Mbadi ni mchapa kazi na ataleta ufanisi mkubwa katika wizara hiyo.

Website | + posts