Home Habari Kuu Mazungumzo ya pande mbili kurejelewa leo

Mazungumzo ya pande mbili kurejelewa leo

0

Mazungumzo kati ya mrengo wa Kenya Kwanza na Azimio la Umoja One Kenya yanarejelewa leo Jumatatu Agosti 21, 2023. Pande hizo mbili zinatarajiwa kukubaliana kuhusu ajenda ya mazungumzo ikikumbukwa kwamba kila upande una mambo ambayo wanaamini ni muhimu.

Makundi hayo mawili yalichagua kamati za kiufundi ambazo kwa pamoja zilijukumiwa kuwianisha ajenda za pande zote kabla ya kurejelea vikao huko Bomas of Kenya.

Kundi la upinzani katika mazungumzo hayo linaongozwa na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka huku kundi la Kenya Kwanza likiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kimani Ichungwah.

Mbunge wa Malindi Amina Mnyazi mmoja wa wawakilishi wa muungano wa Azimio kwenye mazungumzo hayo anasema ajenda zao ni gharama ya juu ya maisha, ukaguzi wa mchakato mzima wa uchaguzi mkuu uliopita, ujumuishi wa wote kwenye masuala ya kitaifa na heshima kwa vyama vya kisiasa.

Upande wa Kenya Kwanza hata hivyo umeapa kuhakikisha masuala hayo hayajadiliwi.

Katika kufichua ajenda za upande wao, Mnyazi amekiuka maagizo waliyopatiwa ya kutojulikanisha ajenda na maafikiano ya mazungumzo hayo.

Huku haya yakijiri, viongozi fulani wa eneo la Ukambani wakiongozwa na mwanachama wa tume ya huduma za bunge Johnston Muthama wanahisi kwamba wakati umewadia wa nchi kusonga mbele ili kupunguza joto la kisiasa.

Baada ya kamati ya mazungumzo kuhalalishwa kupitia bunge, ina siku 60 kujadiliana na kuwasilisha ripoti kwa Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Amolo Odinga.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here