Home Habari Kuu Mawaziri wanne kufika mbele ya bunge la seneti Jumanne

Mawaziri wanne kufika mbele ya bunge la seneti Jumanne

Bunge la Seneti linaandaa vikao vyake Turkana hadi tarehe 29, katika mpango maalum wa ‘Senate Mashinani’ .

0

Mawaziri wanne wanatarajiwa kufika mbele ya Bunge la Seneti siku ya Jumanne, katika kaunti ya Turkana kujibu maswali kuhusu wizara zao.

Bunge la Seneti linaandaa vikao vyake Turkana hadi tarehe 29, katika mpango maalum wa ‘Senate Mashinani’ .

Vikao hivyo vya seneti vinaandaliwa chini ya kipengee cha 126 cha katiba ya Kenya, kinachoruhusu bunge la kitaifa au la seneti kuandaa vikao vyake sehemu yoyote nchini.

Mawaziri watakaofika mbele ya senate ni pamoja na waziri wa usalama wa taifa Kithure Kindiki , Dkt Alfred Mutua wa masuala ya kigeni , Davis Chirchir wa kawi na Salim Mvurya waziri wa madini na uchumi wa majini.

Kamati ya bunge la seneti ilifanya kikao cha kwanza Jumatatu katika kaunti ya Turkana.

Website | + posts