Home Habari Kuu Mawaziri waidhinisha kufutwa kwa madeni ya kampuni za serikali za sukari

Mawaziri waidhinisha kufutwa kwa madeni ya kampuni za serikali za sukari

0

Baraza la Mawaziri kwenye kikao chake rasmi siku ya Jumatatu katika kaunti ya Kisumu, limeidhinisha kufutiliwa mbali kwa madeni yanayodaiwa kampuni za serikali za kusaga miwa kama njia moja ya kuzifufua.

Hazina Kuu pia inapanga kuondoa adhabu ya ushuru na riba ya mikopo kwa viwanda hivyo vya kusaga miwa ambavyo kwa pamoja vina madeni ya shilingi bilioni 117 kupitia kwa mikopo ya benki, malimbikizi ya ushuru na malipo kwa wakulima na wafanyakazi.

Kampuni za sukari za serikali zinadaiwa shilingi bilioni 65 na benki na ushuru wa shilingi bilioni 50 pamoja na madeni ya wakulima na wafanyakazi ya shilingi bilioni 2.

Baraza la Mawaziri pia limeidhinisha maombi ya serikali ya kukodisha viwanda vitano vya sukari ambayo vitachapishwa ndani ya wiki mbili zijazo.

Website | + posts