Home Kimataifa Mawaziri Alfred Mutua na Soipan Tuya waongoza upanzi wa miti Kitui

Mawaziri Alfred Mutua na Soipan Tuya waongoza upanzi wa miti Kitui

Kulingana na mawaziri hao wawili, shughuli hiyo sehemu ya juhudi za serikali za kupanda miti billion 15 ifikapo mwaka 2032.

0
Waziri wa Utalii Alfred Mutua (Kushoto) na mwenzake wa Mazingira Soipan Tuya, wakati wa zoezi la upanzi wa Miti kaunti ya Kitui.

Waziri wa  mazingira, mabadiliko ya hali ya anga na misitu,Soipan Tuya na mwezake wa   utalii na wanyama pori, Dkt. Alfred Mutua, leo Alhamisi waliongoza zoezi la upanzi wa miti katika vilima vya Mumoni, Mwingi,kaunti ya kitui.

Kulingana na mawaziri hao wawili, shughuli hiyo sehemu ya juhudi za serikali za kupanda miti billion 15 ifikapo mwaka 2032.

Akiongea wakati wa shughuli hiyo ya upanzi wa miche, Mutua alisema,kwa kushirikiana na serikali ya kaunti ya Kitui watahakikisha miche iliyopandwa inatunzwa ili ikomae kuwa miti.

“Rasilimali zote zinapaswa kutumia kuafikia asilimia 30 ya utandu wa misitu hapa nchini. Ikiwa lengo hilo halitaafikiwa, kutakuwa na madhara makubwa katika siku zijazo,” alisema waziri Mutua.

Waziri Tuya kwa upande wake alisema lengo la kuja kwake kitui llilikuwa kumsaidia waziri mwenzake anapojitahidi kupanda idadi ya miti aliyopewa katika kaunti za Kitui na Taita Taveta.

Website | + posts