Home Biashara Mauzo ya majani chai katika masoko ya nje yaimarika

Mauzo ya majani chai katika masoko ya nje yaimarika

Gachagua alisema kuwa ufanisi huo umetokana na ushirikiano wa moja kwa moja na washikadau katika sekta hiyo.

0

Mauzo ya majani chai katika masoko ya nje yataongezeka kutoka shilingi bilioni 138 mwaka jana, hadi shilingi bilioni 150 mwaka huu, hayo ni kulingana na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Gachagua alisema wakulima wa majani chai hapa nchini pia watapata mapato yaliyoimarika mwaka huu, baada ya mabadliko yaliyofanyiwa sekta hiyo kuonekana kuzaa matunda.

Kulingana na Naibu huyo wa Rais, malipo ya mwaka huu yatakuwa ya kiwango kikubwa yakilinganishwa na ya miaka iliyotangulia.

Gachagua alisema kuwa ufanisi huo umetokana na ushirikiano wa moja kwa moja na washikadau katika sekta hiyo.

Aliyasema hayo Jumatano alipokutana na wakurugenzi wa Halmashauri ya Ustawi wa Majani Chai Nchini KTDA, katika makazi yake mtaani Karen Jijini Nairobi.

“Matokeo haya katika sekta hii ndogo ya majani chai, ni ya kufurahisha, na yalitokana na mkutano nilioongoza katika kaunti ya Kericho mwezi July mwaka huu,’ alisema naibu wa rais.

Huku akiwataka wakurugenzi hao wa KTDA kuwa na umoja, aliwahimiza kukaza kamba katika kuwahudumia wakulima na kupunguza gharama ya uzalishaji

Website | + posts