Home Habari Kuu Maurice Ogeto mlinzi wa Raila aachiliwa huru

Maurice Ogeto mlinzi wa Raila aachiliwa huru

Mlinzi huyo alitiwa mbaroni Jumatano na kufungwa katika kituo cha Utawala.

0

Mlinzi wa kiongozi wa upinzani Raila odinga-Maurice Ogeto ameachiliwa huru kutoka gerezani.

Akithibitisha taarifa hizo Mkurugenzi wa mawasiliano wa chama cha ODM Philip Etale alisema kuwa Ogeto, aliachiliwa huru mida ya saa saba usiku wa Jumamosi na kuendeshwa kwa gari akiwa amefungwa uso kabla ya kutupwa katika barabara ya Ruiru.

kulingana na Etale gari la Ogeto liliharibiwa huku liking’olewa sehemu kadhaa.

Mlinzi huyo alitiwa mbaroni Jumatano na kufungwa katika kituo cha Utawala.

Ogeto aliachiliwa baada ya mahakama kutoa amri siku ya Ijumaa kuwa afilkishwe mahakamani haraka iwezekanavyo.

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here