Home Habari Kuu Mauaji ya Monicah Kimani: Maribe bado yupo mashakani?

Mauaji ya Monicah Kimani: Maribe bado yupo mashakani?

0

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma amewasilisha ilani ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kumuchilia huru mwanahabari Jacque Maribe katika mauaji ya mfanyabiashara Monicah Kimani.

Kwenye kesi hiyo, Jaji Grace Nzioka alimpata aliyekuwa mpenziwe Maribe, Joseph Irungu almaarufu Jowie na hatia ya kumuua Bi. Kimani.

Hata hivyo, katika hukumu yake iliyotolewa Ijumaa wiki iliyopita, Jaji Nzioka alisema kulikosekana ushahidi wa kutosha wa kumhusisha Maribe na mauaji hayo.

Maribe ni mshatikiwa wa pili katika kesi hiyo ya mauji ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka mitano sasa.

Katika hukumu hiyo, Jaji Nzioka alimtaka Kiongozi wa Mashtaka ya Umma kumfungulia Maribe mashtaka kwa kutoa ushahidi wa uongo kuhusiana na kisa cha ufyatuaji risasi kilichomhusisha Jowie.