Home Habari Kuu Mau Mau wataka bunge kuwasiliana na Uingereza kuhusu fidia

Mau Mau wataka bunge kuwasiliana na Uingereza kuhusu fidia

0

Karani wa bunge la taifa Samuel Njoroge, amepokea rasmi ombi kutoka kwa viongozi wa chama cha waliopigania uhuru wa nchi hii katika vita vya Mau Mau.

Katika ombi lao, wakongwe hao wanapendekeza kutambuliwa kwa wapiganiaji wote wa uhuru na mashujaa wote wa ukombozi wa kitaifa.

Wakiongozwa na Dakta. Gitu Kahengeri, mashujaa hao wa vita vya Mau Mau wanataka bunge liharakishe mchakato wa kuwasiliana na serikali ya Uingereza ili kukamilisha fidia.

wakati wa kikao hicho na karani wa bunge, Daktari Kahengeri, ambaye pia aliwahi kuhudumu kama mbunge wa eneo la Juja, alifichua kwamba viongozi wa kundi lao waliandaa mkutano na Mfalme Charles wa tatu alipozuru Kenya maajuzi.

Kulingana naye, Mfalme Charles alikiri kwamba watu wa nchi yake walitendea wakenya maovu wakati wa ukoloni.

Sasa wanataka wabunge ambao ni wawakilishi waliochaguliwa na wakenya wawasiliane na serikali ya Uingereza kwa niaba yao ili wapate fidia.

Bwana Njoroge alishukuru wazee hao wa Mau Mau kwa kutambua umuhimu wa bunge huku akiwahakikishia kwamba ombi lao litaandaliwa ipasavyo ili kuwasilishwa bungeni rasmi.

Website | + posts